Uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema shirika lina dhamira ya kuendelea kujitanua na kuimarisha miundombinu ya kimkakati ya biashara ikiwemo sekta ya nishati.

Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema hayo katika uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki leo tarehe 26 Mei 2025, Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam.

Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua gari hilo litaongeza ufanisi katika usambazaji wa nishati ya mafuta na kupunguza gharama za usafirishaji hivyo kuongeza mapato ya Shirika.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMAJKT Logistiki Meja Mhidini Nchimbi, amesema gari hilo litatumika kusafirishia mafuta na kusambaza kwenye vituo vya SUMAJKT Energies pamoja na vituo vya watu binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *